Exodus 26:15-25

15“Tengeneza mihimili ya kusimamisha ya mti wa mshita kwa ajili ya maskani. 16Kila mhimili uwe na urefu wa dhiraa kumi
Dhiraa 10 ni sawa na mita 4.5.
na upana wa dhiraa moja na nusu,
17zikiwa na ndimi mbili zilizo sambamba kila mmoja na mwingine. Tengeneza mihimili yote ya maskani jinsi hii. 18Tengeneza mihimili ishirini kwa ajili ya upande wa kusini wa maskani, 19 bkisha tengeneza vitako arobaini vya fedha vya kuweka chini ya hiyo mihimili, vitako viwili kwa kila mhimili, kimoja chini ya kila ulimi. 20Kuhusu upande wa kaskazini wa maskani, tengeneza mihimili ishirini 21na vitako arobaini vya fedha, viwili chini ya kila mhimili. 22Kisha tengeneza mihimili sita kwa mwisho ulio mbali, yaani upande wa magharibi wa maskani, 23na pia utengeneze mihimili miwili ya pembe za upande ulio mbali. 24Katika pembe hizi mbili ni lazima mihimili yake iwe miwili kuanzia chini mpaka juu, na iingizwe kwenye pete moja; mihimili ya pembe hizi mbili itafanana. 25Kwa hiyo itakuwepo mihimili minane, na vitako kumi na sita vya fedha, viwili chini ya kila mhimili.

Copyright information for SwhNEN